WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI (RUWASA) WAMEFANYA KIKAO CHA TATU NA WADAU WA MAJI -UVINZA.
Jumuiya za watumia maji wilaya ya uvinza wakutana katika mkutano mkuu wa tatu na kujadili namna ya kukabiliana na changamoto za maji katika wilaya .
Mkuatano huo umefanyika katika ukumbi wa Makondeko uliopo kata ya Uvinza tarehe 11 mei 2022, wamehudhuria wanajumuiya za watumia huduma za maji na wadau wa maji.
Naye Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Uvinza Boniphace Matete kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Uvinza, amewashukuru wadau wa maji kuhakikisha huduma za maji zinapatikana na pia amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kulinda vyanzo vya maji kwa maslahi mapana ya jamii.
Pia amesisitiza kuwa serikali inahakikisha kuwa kila mwanachi anafunga maji nyumbani katika juhudi za kupambana kumtua ndoa mama kichwani
Afisa Maendeleo ya Jamiii RUWASA wilaya ya Uvinza Joshua Adam akiwamwakilisha meneja RUWASA Uvinza, amebainisha kuwa lengo la RUWASA ni kuhakikisha inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi pia amesisitiza jumuiya za watumia maji kuendelea kusimamia miradi ya maji ili iwe endelevu.
Kaimu Afisa Mazingira wilaya ya Uvinza Nassir Othman amesema wanajumuiya za watumiamaji pamoja na wadau wa maji kuwaa ni jukumu letu sote kuhakikisha utunzaji wa vyanzo vya maji unalindwa na wanajamii wenyewe.
Vilevile Mhasibu wa RUWASA David P. Ngalibaka mkoa Kigoma amewakumbusha Jumuiya ya watumia maji kuhusu usimamizi wa fedha pamoja na ulipaji ankra za maji kwa wakati ili pesa zinazopatikana zisaidie katika ukarabati wa miundo mbinu chakavu katika maeneo yao.
Katika mkutano huo jumuiya za watumia maji wameishukuru RUWASA na serikali kuendelea kutoa huduma ya miundombinu maji ili kuhaikisha wananchi wanaepukana na changamoto ya kero ya maji.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.