Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh. Hanafi Msabaha amepokea mabomba ya Mradi wa Maji .
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Hanafi Msabaha amepokea mabomba ya Mradi wa Maji wa Mlela- Kandaga unaofadhiliwa kuputia fedha za UVICO 19 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji. Jana katika eneo la mradi Mlela.
Meneja RUWASA Wilaya ya Uvinza, Mhandisi Jefta Alphonnce Julius akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Mlela-Kandaga mbele ya Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh. Hanafi Msabaha
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama umefikia hatua za utekelezaji ambapo unategemea kuongezeka kutoka asilimia 51 kwa mwaka 2019 hadi asilimia 59 ifikapo 2021 kuongezeka kwa kupitia fedha za mapambano zidi ya UVICO 19 kutatua changamoto ya wananchi kufikiwa na maji.
Akizungumza na wananchi wa maeneo ya Kandaga na Mlela, Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh.Hanafi Msabaha.
Akikagua mabomba hayo Mh.Hanafi Msabaha Mkuu wa wilaya ya Uvinza amewataka wananchi kushiriki kwenye mradi huo kwa kutunza miundo mbinu ya maji kwa lengo la kufikia ongezeko lililokusudiwa.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Uvinza, Mhandisi Jefta Alphonce Julius akionyesha mabomba ya maji kwa ajili ya Mradi wa Maji Mlela-Kandaga
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.